Home KITAIFA FEI ATAJA SABABU ZA KUONDOKA YANGA,ISHU YA MKATABA

FEI ATAJA SABABU ZA KUONDOKA YANGA,ISHU YA MKATABA

0

KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ameweka wazi kuwa hana tatizo na Yanga bali kuna masuala ambayo amekuwa akifanyiwa na viongozi hayapendi.

Nyota huyo kwa sasa yupo kwenye mvutano na mabosi wa timu hiyo kuhusu suala la mkataba wake ambapo yeye anahitaji kuondoka huku Yanga wakiweka wazi kuwa mkataba wake bado unaishi mpaka 2024.

Fei kwa sasa yupo nje ya uwanja akiwa Zanzibar na ameomba mchango kwa ajili ya kupata fedha ili akafungue kesi mahakama ya michezo ya CAS.

Aidha kwenye mahojiano na moja ya Media Bongo ameweka wazi kuwa hakuna timu ambayo inafanya mazungumzo naye kwa sasa zaidi anachohitaji ni kuwa huru.

“Mimi nimeondoka Yanga kwa sababu ya manyanyaso, mashabiki wa Yanga mimi nawapenda, ila kuna kitu hawakijui ambacho kimenitoa Yanga, kuna aina ya manyanyaso ambayo hayavumuiliki.

“Kuna wakati niliambiwa nauza mechi na baadhi ya viongozi wa Yanga. Siwezi kurudi Yanga kwa sasa kwa kuwa ninahitaji kucheza na kufanya kazi nikiwa huru.

“Nilikaa na viongozi zaidi ya mara mbili kuomba kuvunja mkataba wangu na kwa kuwa kuna kipengele ambacho kinanipa ruhusa ya kuvunja mkataba nilirudisha fedha walizonipa kwa mafungu mara moja,” amesema Feisal Salum.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here