Home KITAIFA HIZI HAPA ZITAKUWA KWENYE KIVUMBI LEO

HIZI HAPA ZITAKUWA KWENYE KIVUMBI LEO

0

KIVUMBI na jasho kinatarajiwa kutimka leo kutokana na mzunguko wa pili kuendelea katika Ligi Kuu Bara 2022/23.

Timu moja tayari imeshashuka daraja ambayo ni Ruvu Shooting inayonolewa Mbwana Makata na mabingwa ni Yanga.

Bado timu moja inasakwa itaungana  Ruvu Shooting Championship na mbili zitacheza hatua ya mtoano.

Kesi ya ubingwa imeshafungwa ambapo mabingwa ni Yanga wametwaa ubingwa wakiwa na pointi 74 baadà kucheza mechi 28.

Ni Singida Big Stars dhidi ya Ruvu Shooting ambayo tayari imeshashuka daraja utachezwa Uwanja wa Liti.

Namungo itamenyana na Dodoma Jiji, Uwanja wa Majaliwa, Tanzania Prisons dhidi ya KMC, Uwanja wa  Nelson Mandela, Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Manungu.

Ihefu dhidi ya Geita Gold itapigwa Uwanja wa Highland Estate, Coastal Union dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Simba dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Azam Complex.

Mbeya City wataikaribisha Yanga ambao ni mabingwa Uwanja wa Sokoine

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here