Home Uncategorized ISHU YA FEI TOTO IMEFIKIA HAPA, TIMU ATAKAYOENDA HADHARANI

ISHU YA FEI TOTO IMEFIKIA HAPA, TIMU ATAKAYOENDA HADHARANI

0

IMEELEZWA kuwa Yanga na Feisal Salum wamekutana kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliweka wazi kuwa angependa kuona mgogogoro baina ya taaisis na Fei Toto unamalizika.

Rais Samia aliwaambia Yanga kwenye hafla ya pongezi ya kutinga fainali Kombe la Shirikisho Afrika na kuwa washindi wa pili Juni 5 kuwa ni aibu kuwa kwenye mgogoro na katoto kadogo.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa hofu ya kumuona anakwenda Simba au kuhakikisha haendi Simba ilikuwa kubwa na habari zikieleza kuwa Simba hawajawahi kuwa wakimhitaji.

Taarifa zimeeleza kuwa Yanga wamelimaza suala la Feisal Salum kwa kuhakikisha anatua Azam FC na imeombwa ilipwe ili atue Azam kiroho Safi kwa kuwa msimamo wa mchezaji umekuwa ni uleule.

Ikiwa dili litakwenda sawa basi Feisal ataitumikia Azam FC msimu ujao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here