Home KITAIFA KIGOGO AFUNGUKA MAYELE KUBAKI YANGA

KIGOGO AFUNGUKA MAYELE KUBAKI YANGA

0

UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi mpango wake wa kushusha vifaa vya maana kwa ajili ya kuhakikisha msimu ujao timu inaendelea kufanya vema ikiwemo kuwabakiza mastaa wake ambao bado wana umuhimu mkubwa kwa timu akiwemo Fiston Mayele.

Hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kumtangaza Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi ambaye amekuja kurithi mikoba ya Nasreddine Nabi.

“Yanga kama viongozi tumefanya kazi nzuri msimu uliopita na tunafurahi kuona timu imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, hivyo ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuhakikisa msimu ujao tunayafikia mafanikio ambayo tuliyafikia msimu uliopita.
“Kikubwa tunachotaka kukifanya ni kuhakikisha tunafanya usajili wa maana ambao utaongeza nguvu kwenye kikosi chetu, lakini pia kuwabakisha wale wote ambao ni muhimu kwa timu, watu wanatakiwa kuwa watulivu na watashuhudia vyuma vya maana vikitua Yanga katika dirisha hili linalokuja la usajili,” alisema kiongozi huyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here