Home KITAIFA KIPA SIMBA SAFARI YAKE SINGIDA FOUNTAIN GATE

KIPA SIMBA SAFARI YAKE SINGIDA FOUNTAIN GATE

0

BAADA ya mkataba wake kugota mwisho ndani ya kikosi cha Simba kipa Beno Kakolanya ameziingiza vitani Azam FC na Singida Big Stars ambayo kwa sasa inaitwa Singida Fountain Gate.

Ni Singida Fountain Gate yenye maskani yake Singida hii inapewa nafasi kubwa kumnasa.

Kipa huyo alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kilichopata ushindi dhidi ya Niger wa kufuzu AFCON ilikuwa Juni 18.

Katika kikosi hicho Kakolanya alianza langoni na ubao ulisoma Tanzania 1-0 Niger bao likijazwa kimiani na Simon Msuva.

Mtu wa karibu wa Kakolanya amesema kuwa Kakolanya ana ofa kutoka timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zilizo ndani ya tano bora.

“Kakolanya kuna timu ambazo zipo kwenye mazungumzo naye hapa Bongo na muda wowote anaweza kutambulishwa ikiwa watafikia makubaliano mazuri.

“Miongoni mwa hizo timu zilizo ndani ya tano bora ni Azam FC, Singida Big Stars pamoja na Namungo suala la muda tu,” ilieleza taarifa hiyo.

Nyota huyo ndani ya kikosi cha Simba alipata nafasi kucheza kwenye mechi mbili za ligi aliposepa na dakika 135.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here