Home KITAIFA KIUNGO HUYU WA KAZI MIKONONI MWA SIMBA

KIUNGO HUYU WA KAZI MIKONONI MWA SIMBA

0

MILTON Karisa nyota mwenye miaka 27 anayekipiga ndani ya Vipers ya Uganda anatakiwa kuwa katika hesabu za Simba.

Kiungo huyo amewahi kufanya kazi na Robert Oliviera ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba ikiwa dili lake litajibu atakuwa miongoni mwa nyota watakaokutana na watani zao wa jadi Yanga kwenye mechi za ushindani.

Yanga ni watani za jadi wa Simba na msimu huu kwenye mechi mbili, Yanga kapoteza moja na kuambulia sare moja katika ligi.

Yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda, ‘The Cranes’ kinachofanya maandalizi ya mechi za kufuzu AFCON 2023.

Nyota huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na timu yake hivyo mabosi wa Simba wanapiga hesabu za kuvunja mkataba wa kiungo huyo.

Oliveira kocha wa Simba kabla ya kuanza mapumziko aliweka wazi kuwa anahitaji kupata viungo na washambuliaji wazuri.

“Tunahitaji kuwa na wachezaji kwenye kila idara na nina amini kwenye eneo la kiungo pia ni muhimu kuwa na viungo wazuri kwa ajili ya uimara wa timu yetu,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here