Home KIMATAIFA KIVUMBI LEO FAINALI FA MANCHESTER UNITED V CITY

KIVUMBI LEO FAINALI FA MANCHESTER UNITED V CITY

0

MENEJA Erik ten Hag amesema Manchester United hawana uwezekano wa kuwa na Antony kwenye fainali ya Kombe la FA Jumamosi dhidi ya Man City.

Itakuwa kivumbi watakapokutana kwenye mchezo huo ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki duniani.

Ten Hag alikuwa na matumaini zaidi kuhusu nafasi ya mshambuliaji wa Brazil baada ya kupata jeraha kwenye mchezo dhidi ya Chelsea.

Mambo bado ni magumu kwa kuwa Antony hajaweza kufanya maendeleo kama ilivyotarajiwa.

Leo Juni 3 Uwanja wa Wembley fainali itafanyika na itakuwa mara ya tatu kukutana kati ya Manchester United na City kwenye Uwanja wa Wembley.

“Antony ana nafasi lakini nafasi ndogo sana licha ya hayo lakini haiwezekani.”

Meneja wa Man City Pep Guardiola amesema:-“Fainali ni jinsi unavyocheza kwa sasa, sio vile ulivyofanya hapo awali, lakini jinsi unavyofanya kibinafsi kama timu.

“Sio muhimu kufikiria yaliyopita au kufikiria miaka mingi iliyopita, ni mchezo mmoja. inabidi tufanye kila tuwezalo.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here