Dili la Real Madrid kupata saini ya nyota wa Dortmund, Jude Bellingham linakaribia kukamilika baada ya kikao kilichofanyika jana baina ya pande zote mbili.
Tayari makubaliano ya mchezaji na Madrid yashakamilika asilimia 100 na wanampango kumalizana nae wiki hii ili wasiingie kwenye vita ya usajili.
Madrid wamepanga kumpa mkataba wa miaka 6 kinda huyo (hadi mwaka 2029).