Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaipongeza klabu ya Yanga kwa hatua ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) akisema ni kanuni pekee imewanyima Kombe hilo lakini waliupiga mwingi.
Majaliwa ameyasema hayo baada ya kupiga simu kituo cha Radio Cha Wasafi wakati Rais wa Yanga Hersi Said akifanyiwa mahojiano asubuhi hii akisema amefurahishwa na hatua kubwa ya Yanga.
Amesema katika mchezo huo wa fainali ya pili uliopogwa juzi nchini Algeria Yanga ilicheza soka kubwa na kufanikiwa kushinda lakini kanuni pekee ndio imewanyima Kombe
“Nawapongeza sana Yanga hakika mlicheza mpira mkubwa na mkafanikiwa kushinda kwa maana kubwa sisi ndio washindi ni kanuni pekee ndio imewanyima kombe lakini tuliwazidi Waalgeria,” amesema Majaliwa
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE