Home Uncategorized MAYELE NA AZIZ KI KUIKOSA AZAM FC, WASEPA NCHINI

MAYELE NA AZIZ KI KUIKOSA AZAM FC, WASEPA NCHINI

0

NYOTA wawili wa Yanga, Fiston Mayele na Stephane Aziz KI watakosa mchezo wa kesho wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mastaa hao ambao wameipatia klabu hiyo ubingwa wa 29 wa Ligi Kuu Bara watakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kwenda kwenye majukumu ya timu zao za taifa zinazocheza michezo ya kufuzu AFCON.

Aziz Ki atacheza mchezo huo wa kufuzu AFCON akiwa na Burkina Faso itakayocheza na Cape Verde huku Mayele anayecheza DR Congo atapambana na Gabon ambapo michezo yote hiyo itachezwa Juni 18.

Mbali na kukosa mchezo huo mastaa hao pia watakosekana katika usiku wa tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) zitakazofanyika siku hiyo jijini Tanga baada ya kuisha kwa fainali ya ASFC.

Kutokana na mastaa hao kukosekana kwenye tuzo hizo watachukuliwa hatua za kinidhamu endapo tu watakuwa hawajatoa taarifa kwenye mamlaka husika ikiwemo kupoteza nafasi ya ushindi, kufungiwa na kupigwa faini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here