Home KITAIFA “MORRISON HANA PUMZI YA KUTOSHA”

“MORRISON HANA PUMZI YA KUTOSHA”

0

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amevunja ukimya juu ya matumizi ya winga Bernard Morrison akisema Mghana huyo hana pumzi ya kutosha kucheza muda mrefu uwanjani. Nabi amesema anatamani kumtumia Morrison kwa muda zaidi pengine kuliko mtu yoyote lakini kutopenda mazoezi makali zaidi ndio kitu kinachomkwamisha kumpa muda mrefu zaidi.

“Watu wengi wanataka kumuona Morrison anacheza lakini sisi makocha ndio tunajua ubora wa kila mchezaji kwa kila dakika kuanzia mazoezini mpaka uwanja wa mchezo,” amesema kocha Nabi nakuongeza;

“Morrison wa Sasa ni vigumu kumpa muda zaidi ya huu tunaompa labda abadalike kwa kujiweka tayari zaidi, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa sana ndio maana tulimleta hapa lakini kwa sasa hayuko tayari kucheza kwa muda mrefu zaidi ya huu tunaompa watu waelewe hili,” amesema Nabi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here