Straika wa zamani wa Orlando Pirates, Bernard Morrison amewaambia Kaizer Chiefs kwanini Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ni chaguo sahihi kwao kwa sasa.
Morrison alinukuliwa na Gazeti la FARPost la Afrika Kusini kwamba; “Anajua kwamba kwenye hizi klabu kubwa,ukipoteza moja na sare moja umeondoka. Kwahiyo anajua presha iliyopo.”
“Amekuwa hapa Yanga kwa karibu miaka miwili, nadhani kwenda kwenye klabu kubwa kama za Afrika Kusini anajua jinsi ya kudili na presha. Anajua kwamba lazima apate matokeo mazuri, kama hatayapata watamtimua.
Habari za uhakika ni kwamba Nabi jana alikuwa kwenye mazungumzo na Kaizer na amewaambia mambo kadhaa anayotaka ikiwemo timu yake ya ufundi na yeye inaelezwa atalipwa donge nono la Sh100milioni anazolipwa Kocha wa sasa ambaye wanataka kumtoa baada ya kushindwa kutimiza malengo.
Nabi amewaambia anataka kwenda na Kocha Msaidizi, Kocha wa Makipa pamoja na mtu wa video na inaripotiwa siku yoyote wiki hii atatua Sauzi kumaliza dili.
Tajiri wa Yanga Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ ameanza hesabu mpya kuanzia leo kuhakikisha anambakiza Nabi na kundi la wasaidizi wake.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga ambazo Mwanaspoti halina shaka nazo ni kwamba GSM atakutana na Nabi kumpa mpango wao ujao ndani ya Yanga ikiwa ni sharti ambalo kocha huyo alitaka kulifahamu baada ya kikosi hicho kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mtihani mkubwa kwa GSM ni kupambana na Wasauzi Kaizer Chiefs ambao Mwanaspoti linafahamu kuwa ndio klabu ambayo inaongoza vita ya kumchukua kocha huyo raia wa Tunisia na amewaambia baadhi ya mastaa kuhusu dili hilo.
Sokaleo.com lilimsaka mtoto wa Nabi, Hedi ambaye amesema”Siwezi kusema anaondoka wala anabaki kwasasa, baba yangu ni mtu anayeheshimu viongozi mashabiki na hata wachezaji wake lakini kitu ambacho kitakwenda kutoa picha halisi ya baadaye ni pale atakapokutana na uongozi wa klabu yake,”.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE