Home KITAIFA NABI AFUNGUKIA ISHU YA MABAO KIMATAIFA

NABI AFUNGUKIA ISHU YA MABAO KIMATAIFA

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kufungwa kwa timu hiyo kutokana na mipira ya adhabu ni sehemu ya mpira.

Yanga ikiwa imefungwa mabao 7 kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, kuanzia hatua ya makundi mpaka fainali imefungwa mabao matano yaliyotokana na mapigo huru.

Miongoni mwa mabao ambayo walifungwa yaliyotokana na mapigo huru ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe, Real Bamako, US Monastri mabao mawili na dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa fainali.

Katika mabao hayo yote hakuna pigo la penalti bali ni faulo pamoja na kona kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Real Bamako.

Nabi amesema kuwa kwenye mpira hakuna timu ambayo haitafuti ushindi ndani ya dakika 90.

“Hakuna timu ambayo haitafuti matokeo ambacho kimetokea kwa kufungwa mabao ya adhabu ni makosa kwenye mpira na ipo wazi kuwa mpira ni mchezo wa makosa,” amesema Nabi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here