Home KITAIFA NDOYE APEWA MKATABA AZAM FC

NDOYE APEWA MKATABA AZAM FC

0

PAPE Malickou Ndoye nyota wa Azam FC ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kubaki ndani ya timu hiyo.

Nyota huyo raia wa Senegal amekuwa na kazi kubwa katika timu hiyo ambayo imekamilisha ligi ikiwa nafasi ya tatu.

Taarifa rasmi kutoka ndani ya Azam FC imeeleza kuwa nyota huyo ambaye ni beki kitasa bado yupo ndani ya kikosi hicho.

Anaungana na kocha wake wa zamani Youssouph Dabo ambaye naye ni raia wa Senegal atakayeinoa timu hiyo kwa msimu 2023/24.

Azam FC inafanya maboresho ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo kwa msimu wa 2022/23 mabingwa ni Yanga.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here