Home KITAIFA NGUMU KUIKATAA DAWA, FUNGA MSIMU YA KILIO NA TABASAMU

NGUMU KUIKATAA DAWA, FUNGA MSIMU YA KILIO NA TABASAMU

0

NGUMU kuikataa dawa pale ugonjwa unapozidi ipo hivyo kutokana na kila mmoja kupambania malengo yake.Msimu umefungwa kwa jasho, kilio na tabasamu kwa waliofikia mipango yao.

Msimu wa 2022/23 umefungwa na kila kitu kimeshuhudiwa ndani ya uwanja kwa timu kupambana huku Polisi Tanzania na Ruvu Shooting hawa wakianza maisha mapya ndani ya Championshi.

Hapa tunakuletea baadhi ya rekodi zilivyoandikwa namna hii:-

17

Nyota wa Yanga Fiston Mayele mchezo wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons alitupia bao moja dakika ya 33 akitumia pasi ya Salim Aboubhakari, ‘Sure Boy’.

Ni bao lake la 17 msimu wa 2022/23 akiitibua rekodi yake mwenyewe alipokuwa Yanga aliyopachika msimu wa 2021/22 alipofunga mabao 16 kibindoni na kinara alikuwa ni George Mpole aliyekuwa anakipiga Geita Gold.

Mayele anafikisha mabao 17 kwenye ligi akivunja rekodi yake aliyoiandika mwenyewe msimu wa 2021/22 alipofunga mabao 16.

Ntibanzokiza

Saido Ntibanzokiza nyota wa Simba katupia maao mawili kwenye mchezo wa kufungia msimu wa 2022/23 dhidi ya Coastal Union ilikuwa dakika ya 13 na 73 akikiwa sana na Mayele wa Yanga.

Nyota huyo dakika ya 13 ilikuwa ni kwa pigo huru na dakika ya 73 kwa pasi ya mshikaji wake Shomari Kapombe ilikuwa Uwanja wa Uhuru.

Kipigo kikubwa

Msimu wa 2022/23 umefungwa kwa ushindi mkubwa ambapo ni Azam FC walioshuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complec ukisoma Azam FC 8-0 Polisi Tanzania

Prince Dube katupia mabao manne ikiwa ni dakika ya 8, 15, 28, 56,  Kipre Junior alifunga bao dakika ya 20 huku Idd Suleiman yeye akitupia mabao mawili dakika ya 40 na 75 mwamba Zayha Zayd alipachika bao dakika ya 85.

Dube ni nyota wa kwanza kufunga hat trick ndani ya Azam FC kwa msimu wa 2022/23 akifikisha jumla ya mabao 12.

Mwendo wa 10

John Bocco nahodha wa Simba mchezo wake wa kufungia msimu alipachika bao ilikuwa dhidi ya Coastal Union dakika ya 56 akifikisha mabao 10 kibindoni.

Moses Phiri kagotea kwenye namba 10 ya mabao baada ya kutokuwa nje kwa muda mrefu kwa kuwa hakuwa fiti.

Bruno Gomes nyota wa Singida Big Stars kibindoni katupia mabao 10 akiwa ni kinara ndani ya timu hiyo na bao lake la 10 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Liti.

 9 zimekusanywa tano

Mastaa watano ndani ya ligi wamefunga msimu wakiwa na mabao 9 kibindoni ndani ya ligi.

Sixtus Sabilo wa Mbeya City, Stephen Aziz Ki wa Yanga, Pape Sakho wa Simba, Collins Opare wa Dodoma Jiji na Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons.

KMC na Mbeya City

Walikutana kwenye beto ya mwisho walipokuwa wakisaka pointi tatu Uwanja wa Nelson Mandela huku KMC wakisepa na pointi tatu mazima.

Licha ya KMC kushinda wanagotea kwenye nafasi kucheza hatua ya mtoano kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi.

KMC inagotea nafasi ya 13 ikiwa na pointi 32 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 14 pointi zake ni 31 zote zikiwa zimecheza mechi 30.

Tano tu zimegawa ubingwa

Mabingwa wa ligi ni Yanga wakiwa wamekusanya pointi 78 baada ya kucheza mechi 30 huku Simba wakiwa na pointi 73 tofauti ni pointi tano.

Pointi tano zimetofautisha hesabu za ubingwa ambao ni wa pili mfululizo kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here