Home KITAIFA NIFUATE YA SAMAKI YAPAMBA MOTO

NIFUATE YA SAMAKI YAPAMBA MOTO

0

KWENYE Nifuate ya Samakiba huku mgeni rasmi akiwa ni rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amekuwa shuhuda ubao ukisoma Timu Samatta 4-2 Timu Kiba.

Mchezo huo wa hisani maalumu kwa ajili ya kurejesha kwa jamii umepamba moto huku kila mmoja akionesha ujuzi wake ndani ya uwanja.

Mchezo huo wa hisani ulichezwa Uwanja wa Azam Complex na mashabiki walijitokeza kwa wingi.

Mbwana Samatta nahodha wa Timu Samatta amesema kuwa hawakukamia mchezo huo walicheza kawaida lakini wameshinda.

Ni John Bocco alifungua ukurasa wa kufunga dakika ya 21 kisha Sopu akafunga tatu dakika ya 45,63 na 71.

Kazi ya Kiba ilikutana na Ayoub Lyanga dakika ya 69 akafunga bao la kwanza na kamba ya pili dakika ya 90+4 kazi ya Marioo.

“Unadhani tulicheza kwa kumaanisha sana mchezo wetu hapana nadhani watazamaji wao wanaona kwamba tulicheza kwa nguvu kubwa.

“Uwanjani wachezaji tulikuwa tunacheka na kuzungumza kawaida kabisa hili kwetu ni jambo jema na kwa wote waliojitokeza tunasema asante,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here