Home KITAIFA ORODHA YA MASTAA THANK YOU YAONGEZEKA MSIMBAZI

ORODHA YA MASTAA THANK YOU YAONGEZEKA MSIMBAZI

0

GADIEL Michael beki wa kushoto wa kikosi cha Simba msimu wa 2022/23 mkataba wake umegota mwisho na mabosi wa timu hiyo wamempa mkono wa asante.

Beki huyo mzawa aliibuka ndani ya Simba akitokea kikosi cha Yanga 2019/20 ambapo amedumu kwenye kikosi hicho kwa misimu mitatu.

Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 baada ya kukamilisha msimu wakiwa na pointi 78 kibindoni.

Ni pointi tano wamekuwa tofauti Yanga na Simba kwenye ligi kwa kuwa Simba ambayo imeongeza orodha ya mastaa waliopewa mkono wa asante ilikusanya pointi 73.

Msimu wa 2022/23 hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu Roberto Oliveira raia wa Brazil na alipata nafasi ya kucheza mechi 4 akitumia dakika 182.

Anaungana na nyota wengine ambao hawatakuwa ndani ya kikosi cha Simba ikiwa ni pamoja na Agustino Okra, Nelson Okwa, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Beno Kakolanya, Victor Akpan.

Taarifa iliyotolewa na Simba ilieleza:”Uongozi wa klabu unapenda kuwajulisha kuwa hatutaendelea kuwa na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael baada ya mkataba wake kufikia tamati,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here