Shirikisho la soka duniani FIFA limethibitisha kuwa michuano ya kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu mwaka huu 2023 itafanyika katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia.
Uamuzi huo umefikiwa kufuatia ziara ya wajumbe wa FIFA mjini Jeddah kukagua maandalizi yanayoendelea kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 22 Desemba 2023. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu kufanyika nchini Saudi Arabia.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE