Home KITAIFA SIMBA WAJA NA GIA NYINGINE, MSIMU UJAO MTAISOMA NAMBA

SIMBA WAJA NA GIA NYINGINE, MSIMU UJAO MTAISOMA NAMBA

0

ROBERTO Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini timu hiyo itakuwa kwenye mwendo mzuri msimu ujao ikiwa itapata wachezaji wenye ubora kila idara.

Kocha huyo alikiongoza kikosi cha Simba kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Yanga Uwanja wa Mkapa.

Henock Inonga na Kibu Dennis hawa ni nyota waliofunga mabao kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi imegotea nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 67 huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi 74.

Katika mechi 9 za ligi ambazo alikaa benchi alipochukua mikoba ya Zoran Maki ni mechi 7 alishinda na mbili akiambulia sare.

Sare zote ilikuwa ni kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC pamoja na ule wa Namungo.

Kocha huyo amesema:”Ambacho tunapaswa kufanya kwa sasa ni kutulia na kufanya maandalizi mazuri kwa msimu ujao kwani hii ni timu kubwa na bora.

“Wachezaji wetu wana vipaji na wanajituma kwenye majukumu yao hiyo ni furaha kwetu na ambacho tunahitaji ni kupata matokeo,”.

Simba kwa sasa inafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here