SIMBA ipo kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilisha usajili wa mfungaji bora wa Ligi Kuu Rwanda, Leandre Essomba Willy Onana, Sokaleo inafahamu.
Straika huyo wa Rayon Sports tayari ameshatua Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha dili hilo la kuja kuichezea miamba hiyo ya Msimbazi kwa msimu wa 2023-2024.
Kinara huyo wa mabao kwa msimu wa 2022-23, alitikisa nyavu mara 16 kwenye ligi na kinachoelezwa tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya jana Jumapili na asubuhi ya leo Jumatatu anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kukipiga kwa Wekundu hao wa Msimbazi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE