Home KITAIFA TAIFA STARS KAZI INAENDELEA

TAIFA STARS KAZI INAENDELEA

0

MBWANA Samatta nyota anayepambania nembo ya Tanzania katika Klabu ya Genk ya Ubelgiji ni miongoni mwa walioanza mazoezi na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Adel Amrouche imeanza maandalizi kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, (AFCON).

Ni Jumapili Juni 18 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa dhidi ya Niger ukiwa ni mchezo wa tano wa kusaka tiketi ya kufuzu AFCON utakaopigwa Uwanja wa Mkapa.

Mbali na Samatta katika orodha ya mastaa 30 walioitwa kupambania nembo ya Tanzania wapo wengine kutoka Yanga, Simba, Singida Big Stars, Coastal Union.

Baadhi ni Beno Kakolanya kipa namba mbili wa Simba, Metacha Mnata kipa namba tatu wa Yanga, Dickson Job beki wa Yanga, Raphael Daud kutoka Ihefu, Aziz Andambwile kutoka Singida Big Stars.

Stars ipo kundi F la mashindano ikiwa na timu za Uganda, Algeria na Niger ni nafasi ya tatu na poiñti nne kibindoni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here