Arsenal itaongeza juhudi za kumnunua Declan Rice kwa pauni milioni 92 kwa matumaini kwamba kiungo huyo wa West Ham na Uingereza, 24, anaweza kujiunga kwa wakati kwa kabla ya kuanza kwa msimu. (Telegraph – usajili unahitajika)
West Ham wanapania kumleta kiungo mkabaji wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 27, kuchukua nafasi ya Rice, huku Manchester City na Kalvin Phillips wa Uingereza na kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse pia wakiwa kwenye orodha hiyo. (Mail)
Chelsea pia huenda wakamsajili Rice pamoja na kiungo wa kati wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21. (90min).
Mchezaji wa Nice na Ufaransa Khephren Thuram, 22, amekubaliana kwa maneno na Liverpool. (Football Transfers)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Croatia Mateo Kovacic, 29, amekubali masharti ya kibinafsi na Manchester City baada ya kupiga hatua katika mazungumzo ya usajili. (Fabrizio Romano)
Liverpool wamepanga mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Manu Kone, 22. (Fabrizio Romano)
Real Madrid wanafanyia kazi dau la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane kwa takriban £68m huku mwenyekiti wa Tottenham Hotspur Daniel Levy akikataa kumuuza mchezaji huyo wa miaka 29 kwa Manchester United. (Marca kwa Kihispania)
Newcastle wanatafakari uwezekano wa kuwasajili wachezaji kutoka kwa timu zilizoshushwa daraja katika Ligi ya Primia akiwemo kiungo wa Leeds United na Marekani Tyler Adams, 24, na winga wa Leicester City Muingereza Harvey Barnes, 24, na kiungo James Maddison, 26. (Telegraph).
Maddison ananyatiwa na meneja mpya wa Tottenham Ange Postecoglou, lakini klabu hiyo italazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 50 kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Telegraph – usajili unahitajika)
Kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 32, analengwa na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain. (L’Equipe – kwa Kifaransa)
Klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia imeelezea nia yao ya kutaka kumsajili winga wa Algeria Riyad Mahrez, 32, kutoka Manchester City. (Fabrizio Romano)
Tottenham watahitaji kuongeza dau lao la pauni milioni 20 kama wanataka kumsajili kipa wa Uhispania David Raya, huku Brentford wakiwa tayari kukataa ofa ya chini ya pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (i Sport)
Arsenal wanamuona beki wa Kihispania, 18, Ivan Fresneda wa klabu ya La Liga ya Valladolid kama chaguo bora la majira ya joto. (Football London)
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE