Home KITAIFA UTAWALA WA WAGENI UTAZAMWE KWA UMAKINI

UTAWALA WA WAGENI UTAZAMWE KWA UMAKINI

0

MUDA mchache wanasema mambo ni mengi ila ili yote yaende kwa umakini jambo la muhimu kuzingatia ni mpangilio kwenye kila hatua.

Ni kuanzia Singida Big Stars ambao wamekuwa na msimu mzuri ndani ya Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza wanapaswa kuwa na mwendelezo.

Kwa sasa Singida Big Stars inaitwa Singida Fountain Gate FC hivyo ni muhimu kuendelea pale ambapo waliishia.

Yanga pia nao wanahusika mpaka Kagera Sugar bila kuwasahau Namungo timu zote umakini unahitajika.

Ipo wazi kwamba hakuna muda wa ziada ukishapita hata ikiwa ni dakika moja hautakutana nayo tena wakati wowote ule wa sasa ama ule ujao.

Hivyo ikiwa hakuna muda wa ziada ni muhimu kufanyia kazi makosa ambayo yamepita hasa kwa msimu wa 2022/23 ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Kwenye kila idara katika timu mbalimbali zimeonyesha makosa yao hasa kwenye eneo la ushambuliaji.

Hili linawahusu wazawa wao wamekuwa kwenye mwendo wa kupanda na kushuka wanapokuwa uwanjani jambo linalowapa nafasi wageni kuwa na mwendelezo bora.

Haina maana kwamba wazawa hawajafanya kazi kubwa kwenye eneo la ushambuliaji hapana lakini wamepotezwa na wageni kwenye namba.

Wakati ujao hapo ni muhimu kufanya kazi kubwa katika idara hii ili kila kitu kiwe sawa na ushindani uzidi kuwa mkubwa.

Katika sekta ya ulinzi ni deni ambalo linabaki kwa mabeki wazawa kwa kuwa kasi yao imekuwa bora licha ya kuvutana mashati na wachezaji wakigeni.

Tumeona kila timu inafanya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi na hilo linaongeza umakini kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake.

Jambo la msingi kwenye sekta ya ulinzi izidi kuwa imara kwa timu zote kwani kwenye upande wa mlinda mlango inaonekana utawala mpya wa wageni unazidi kutawala.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here