Home KITAIFA WATATU WAPENYA TUZO SIMBA, SAIDO NDANI

WATATU WAPENYA TUZO SIMBA, SAIDO NDANI

0

KWENYE orodha ya Wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) mwezi Mei, 2023 kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza jina lake limepenya.

Ntibanzokiza anapambania tuzo hiyo akiwa kiungo peke yake huku wawili wakiwa ni mabeki wa kazikazi ndani ya Simba.

Nyota huyo kafunga msimu akiwa ametupia mabao 17 sawa na nyota Fiston Mayele wa Yanga.

Ishu ya nani atakuwa mfungaji bora kamati imeweka wazi kuwa itakaa kujadili hivyo itafahamika kama kiatu kitakwenda Yanga ama Simba au namna watakavyoamua.
Ni Henock Inonga beki wa kazi ngumu nae yupo kwenye orodha pamoja na Shomari Kapombe beki wa kumwaga majalo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here