Home KITAIFA WINGA WA KAZI IMEISHA HIYO YANGA

WINGA WA KAZI IMEISHA HIYO YANGA

0

KUTOKA Dodoma mpaka Dar kutokana na uwezo wake ambao uliwavutia mabosi wa Yanga wakampa dili kuitumikia timu hiyo.

Alikuwa anacheza ndani ya Dodoma Jiji akaanza changamoto mpya Yanga yenye maskani yake Jangwani, Kariakoo.

Mafanikio makubwa akiwa na timu hiyo ni pamoja na kuwa miongoni mwa wachezaji walioandika historia ya kutinga hatua ya fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika ni rekodi yake kubwa kuliko akiwa na Yanga.

Anaitwa Dickson Ambundo winga mwenye uwezo mkubwa wa kutumia mguu wa kulia katika kufanya kazi yake aipendayo ya mpira.

Nyota huyo chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi hakuwa chaguo la kwanza kikosi cha Yanga kutokana na ushindani wa namba ambao ulikuwa ndani ya kikosi hicho.

Yanga imetwaa Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara, Kombe la Azam Sports Federation naye akiwa ni miongoni mwa wale waliovaa medali.

Msimu ujao 2023/24 hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga ameambiwa Thank You hivyo winga matata ndani ya Yanga imeisha hiyo unaweza kusema.

Yanga wamemshukuru na kumtakia kila la kheri huko aendako.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here