Home KITAIFA YANGA HATARINI KUFUNGIWA USAJILI, EYMAEL AMESEMA ASILAUMIWE

YANGA HATARINI KUFUNGIWA USAJILI, EYMAEL AMESEMA ASILAUMIWE

0

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara na Kombe la ASFC, Yanga wanaweza kukumbana na rungu la kufungiwa kusajili katika madirisha matatu ya usajili ikiwa ni pamoja na kuondolewa msimu ujao kwenye michuano ya Kimataifa.

Uamuzi huo unaweza kufanywa muda wowote, kutokana na Yanga kushindwa kulipa kwa wakati deni la aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Luc Eymael aliyeiburuza Yanga FIFA kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake miezi michache baada ya kibarua chake kuota nyasi, Septemba 2021.

Hata hivyo miamba hiyo ya soka la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki ilikubali kumlipa kocha huyo kwa awamu.

Kwa mujibu wa notisi ya malipo ya Eymael, Yanga ilipaswa kumalizana naye ndani ya siku 45 huku kuanzia Juni 9 mwaka huu wakitakiwa kulipa na riba ya asilimia tano hadi juzi Ijumaa ambapo ilikuwa siku ya mwisho kumaliza deni la Dola 66,000 ambazo ni zaidi ya Sh157 milioni.

Kocha huyo, ameliambia Mwanaspoti kuwa asilaumiwe kwa kile ambacho FIFA inaweza kufanya kufuatia Yanga kushindwa kukamilisha kile ambacho walikubaliana kuhusu malipo yake kwani hadi siku ya mwisho, juzi walikuwa wamemlipa nusu ya kiwango ambacho alitakiwa kupata.

“Nimekuwa nikifanya nao mawasiliano lakini naona wamekuwa kimya, kwa kuwa hili suala limefika kwenye mamlaka husika kwa hiyo tutaona kile ambacho wataamua, wanaweza pia kuingia kwenye adhabu ya kupokonywa pointi tisa,”
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alitafutwa kutoa ufafanuzi wa jambo hilo, lakini simu yake haikupokelewa sawa na ilivyokuwa kwa Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here