Home KIMATAIFA YANGA KAMILI KUWAVAA WAARABU KIMATAIFA

YANGA KAMILI KUWAVAA WAARABU KIMATAIFA

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa watafanya kazi kubwa kwenye mchezo dhidi ya USM Alger kwenye fainali ya pili ugenini.

Waarabu hao wa Algeria wanafaida ya mabao mawili waliyopata ugenini mbele ya Yanga huku mtupiaji wa bao la Yanga akiwa ni Fiston Mayele.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-2 USM Alger.

Miongoni mwa wazawa ambao walipata nafasi ya kuanza kwenye fainali ya kwanza na kuandika rekodi nzuri ni beki wa kazi Dickson Job pamoja na Bacca ambao walikuwa kwenye kutimiza majukumu yao.

Nabi amesema:”Tunaka kazi kubwa kwa ajili ya kutafuta ushindi ninajua watu wa mpira wanajua kwamba bado kazi haijaisha hivyo tutapambana,”.

Tayari kikosi kipo Algeria kwa sasa na Juni 2 wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa leo majira ya saa 4.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here