Home KIMATAIFA YANGA PATUPU KWA MOSIMANE, ATAMBULISHWA UARABUNI

YANGA PATUPU KWA MOSIMANE, ATAMBULISHWA UARABUNI

0

Klabu ya Al Wahda πŸ‡¦πŸ‡ͺ ya Abu Dhabi huko Umoja wa Falme za Kiarabu inayoshiriki Ligi kuu ya UAE imemtangaza aliyekuwa kocha wa Al Ahly πŸ‡ͺπŸ‡¬, Pitso Mosimane kama kocha mkuu klabuni hapo.

Mosimane (54) raia wa Afrika Kusini aliachana na klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia kutokana malimbikizo ya mishahara yake tangu Januari mwaka huu.

Aliifundisha Al Ahli πŸ‡ΈπŸ‡¦ kwa miezi 8 na kuiongoza kupanda hadi ligi ya Kuu Nchini humo huku akiiongoza kutwaa Ubingwa wa ligi daraja la kwanza.

Habari hizi zinazima zile zilizokuwa na uwezekano mdogo sana kuwa kweli kwamba huenda mkufunzi huyo mashuhuri barani Afrika angekuja kukiwasha hapa Tanzania.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here