KLABU ya Simba imetangaza kukamilisha usajili wa Kiungo Abdallah Hamisi kwa kandarasi ya miaka miwili.
Nyota huyo wa zamani wa timu za Muhoroni Youth Fc, Bandari Fc na Sony Sugar za Kenya amejiunga na Simba akiwa mchezaji huru.
Kupitia kurasa za mitandao za timu hiyo imechapishwa taarifa ya kuinasa saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania.
Mchezaji huyo anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa Julai 20, 2023 baada ya mapema Shabani Iddi Chilunda kutambulishwa msimbazi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE