Home HABARI AIR MANULA MDOGOMDOGO ANAREJEA

AIR MANULA MDOGOMDOGO ANAREJEA

0

AISHI Manula, ‘Air Manula’ kipa namba moja wa Simba taratibu anazidi kurejea kwenye uimara wake baada ya kuwa kwenye mwendelezo wa matiabu ya afya yake.

Ikumbukwe kwamba kipa huyo ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Roberto oliveira hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza Kariakoo Dabi ya mzunguko wa pili ni mikono ya kipa namba tatu Ally Salim ilikuwa langoni dhidi ya watani wa jadi Yanga.

Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 Yanga ukiwa ni mchezo wa pili kwa Yanga kupoteza ndani ya ligi msimu wa 2023/24.

Manula amesema kuwa taratibu anarejea kwenye ubora wake baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Ihefu ambao ulikuwa ni wa Kombe la Azam Sports Federation.

“Kila hatua dua” ni neno la Air Manula la hivi karibuni baada ya kupata matibabu.

 

Kwa sasa ni Ally Salim ndiye mbeba mikoba ya Manula kambini Uturuki ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Inatajwa kwamba Simba ipo kwenye hesabu za kumsaka kipa mwingine ambaye atakuja kuongeza nguvu katika eneo hilo.

Mpaka sasa Simba imesajili mabeki na viungo kwa ajili ya msimu wa 2023/24 huku ikitajwa kumleta kipa kutoka nje ya Tanzania.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here