Home KITAIFA CHAMA AFUNGUKA MAZITO BAADA YA KUTUA KAMBINI UTURUKI, KUHUSU KIMATAIFA FULL MIKWARA

CHAMA AFUNGUKA MAZITO BAADA YA KUTUA KAMBINI UTURUKI, KUHUSU KIMATAIFA FULL MIKWARA

0
chama

Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa usajili walioufanya na kukiri kuwa wana kikosi cha mataji msimu ujao.

Chama, ambaye ameungana na wenzake nchini Uturuki ambako Simba SC imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya 2023/24, amekiri kuwa wanakikosi kizuri na ushindani.

“Tupo kwenye maandalizi ya msimu mpya kuna wachezaji wengi wapya tunapambana kuhakikisha tunatengeneza muunganiko mzuri ambao utakuwa na tija ndani ya timu msimu ujao;

“Lengo ni kuhakikisha tunamaliza msimu tukiwa na mataji muhimu, ambayo yataturejesha kwenye ushindani hasa kimataifa ambako tunatamani kuvuka hatua ambazo tayari tumezipiga kwa misimu minne mfululizo, hilo linawezekana tukiendeleza juhudi zetu na kuwa wamoja.” amesema.

Chama amesema wachezaji ambao wameosajiliwa Simba SC wote ni wazuri, na anaamini watakuwa chachu ya wao kuwa bora zaidi ya msimu uliopita hawakufanikiwa kutwaa taji hata moja.

Kiungo huyo mshambuliaji hakusita kummwagia sifa mshambuliaji wao mpya, Willy Onana, ambaye alikiri kuwa ni moja ya sajili bora zilizofanyika ndani ya timu hiyo, huku akikiri kuwa mabao mengi yatafungwa.

“Si sahihi kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja kama nilivyozungumza hapo mwanzo kuwa usajili uliofanywa ni wa kuwapongeza viongozi na ni kazi kwetu kuwafanyia kilocho bora.

“Onana kama unavyotaka nimzungumzie ni mchezaji mzuri anajua kukaa kwenye nafasi, atafunga sana msimu ujao, ameonyesha kuwa na kitu kwenye mguu wake, anapenda kufunga, Simba SC itafunga mabao mengi msimu ujao, japo ni kawaida kwetu,” ameongeza Chama.

Akimzungumzia kurudi kwa Luis Miquissone, amesema amefurahi na anaamini atafanya mambo makubwa, huku akikiri kuwa alikuwa akiwasiliana naye mara kwa mara kuhusu mpira.

Katika hatua nyingine, Mlinda Lango raia wa Brazil, Jefferson Luis ametambulishwa kuwa mbadala kuwa wa Beno Kalolanya aliyetimkia Singida Fountain Gate.

Jefferson Luis atampa changamoto Aishi Manula katika kuwania nafasi ya Mlinda Lango chaguo la kwanza katika kikosi cha Simba SC msimu ujao 2023/24.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here