Home KITAIFA CHEKI JONAS MKUDE NAMNA ALIVYOANZA KAZI

CHEKI JONAS MKUDE NAMNA ALIVYOANZA KAZI

0

KIUNGO mpya wa Yanga, Jonas Mkude ameanza kazi kuelekea msimu mpya wa 2023/24.

Safari huu Mkude mzawa mwenye uwezo eneo la kiungo atakuwa na uzi wa Yanga baada ya kuibuka hapo akiwa huru.

Nyota huyo alipewa mkono wa asante na Simba timu ambayo amecheza kwa muda wa miaka 13 kwenye soka la ushindani na kujiunga na Yanga.

Simba ilipompa mkono wa asante akapata dili kwa watani wa jadi Yanga hivyo bado yupo mitaa ya Kariakoo Mkude.

Tayari timu ya Yanga imeanza maandalizi ikiwa imeweka kambi Kigamboni kuelekea msimu mpya.

Julai 22 ni Wiki ya Mwannachi na Yanga natarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs.

Katika mazoezi yao kiungo Bernard Morrison ambaye naye kwa sasa ni huru baada ya kupewa mkono wa asante aliwatembelea kwenye mazoezi hayo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here