Home KITAIFA FEI TOTO AFUNGUKA KITU ATAKACHOIFANYIA AZAM, AWAAMBIA HAYA WACHEZAJI WENZAKE

FEI TOTO AFUNGUKA KITU ATAKACHOIFANYIA AZAM, AWAAMBIA HAYA WACHEZAJI WENZAKE

0

KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema amezungumza na wachezaji wenzake kikosini hapo na kukubaliana kufikia malengo yao msimu ujao wa 2023/24 ikiwa ni pamoja na kupata ushindi kwenye mechi zao.

Fei Toto amesajiliwa na Azam FC akitokea Yanga, ataanza changamoto mpya kwenye kikosi hicho msimu wa 2023/24.

Timu hiyo ambayo itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Youssouph Dabo raia wa Senegal na msaidizi wake, Mfaransa, Bruno Ferry wameanza maandalizi ya msimu wa 2023/24, leo Jumapili inatarajia kueleka jijini Sousse nchini Tunisia kwa ajili ya kambi ambayo itaanza Julai 9 hadi 30, 2023.

Akizungumza na Spoti Xtra, kiungo huyo amesema: “Tupo na wachezaji wengine ambao ni wapya kwenye kikosi, tumezungumza kwa pamoja kuona namna gani tunafikia malengo ambayo tunahitaji kuyafikia, tutapambana kufanya vizuri.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here