Home KITAIFA ISHU YA MAYELE KUONDOKA AU KUBAKIA YANGA IKO HIVI

ISHU YA MAYELE KUONDOKA AU KUBAKIA YANGA IKO HIVI

0

Licha ya kufanya siri kubwa, lakini sokaleo.com imevidaka za chini ya kapeti kuwa vigogo wa Yanga juzi usiku walikuwa na kikao kizito na Fiston Mayele nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na ufukwe wa Bahari ya Hindi

Kikao hicho kilihusisha pia wasimamizi wa mchezaji huyo ambao wanapushi staa huyo akakiwashe Arabuni ambako kuna mkwanja mnene na wako tayari kununua mkataba uliosalia Yanga.

Bado hawajafikia muafaka wa kusalia au kuondoka ingawa tajiri kaahidi dau nono lakini jana mchana pia Mayele alionekana sehemu akipiga picha za matangazo ya uzi mpya wa Yanga jambo ambalo linaashiria lolote linaweza kutokea na akaonekana ameshikilia uzi mpya wa Jangwani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here