Tunachoweza kuwaza juu ya mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta ni juu ya uwezo wa soka hivi sasa.
Kandarasi yake imehamia katika klabu Panthessalonian Athletic Club of Constantine Politans P. A. O. K inayoshiriki ligi kuu ya Ugiriki.
Anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Afrika kujiunga na vigogo hawa wa soka waliomaliza nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Ugiriki 2022/2023 Samatta anaungana na waafrika wenzake Baba Rahman kutoka Ghana na Wiliam Trost Ekong kutoka Nigeria.
Lakini je kiwamgo cha Sammata katika soka la bara la ulaya kinaporomoka ama kinapanda ?
Samatta Ametoka kwenye ligi namba 5 kwa ubora barani ulaya ligi kuu ya ubelgiji na kwenda kwenye ligi namba 18 Kwa ubora barani ulaya je ni kweli kiwango kimeporomoka ?
Kuhama kutoka katika klabu inayoshika nafasi ya 107 barani ulaya (KRC GENK) na kuhamia kwenye klabu inayoshika nafasi ya 97 barani ulaya (PAOK) inatosha kuonesha ubora wa kiwango.
Je ni mafanikio ya timu ndo yatatuwezesha kujua ubora wa kiwango cha Sammata?
Ama ushiriki wa vilabu katika michuano makubwa ya kimataifa ndio jambo ambalo litatosha kupima ubora wa samatta?
Kijana Mtanzania Mbwana Ally Samatta ni moja kati ya wachezaji wenye uchezaji mzuri wanapokua uwanjani lakini hatuwezi kujua hatma ya soka lake.
Wewe unaona nini juu ya uhamisho huu wa Samatta kuelekea klabu ya PAOK kutoka Ubelgij?
Usisahau kutofollow kwenye page yetu ya instagram kama sokaleotz