Home KITAIFA KMC KUPITA NA “THANK YOU” KWA NYOTA WAKE 11

KMC KUPITA NA “THANK YOU” KWA NYOTA WAKE 11

0

BAADA ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa ushindi kwenye mchezo wa mtoano KMC imewaandikia mastaa 11 barua za kuwapa mkono wa Thank You.

Ni Yanga wamesepa na ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2022/23 hivyo KMC nao wanapiga hesabu za kufanya vizuri katika msimu ujao.

Ipo wazi kwamba kwenye mechi waliyokutana na Yanga mzunguko wa pili Uwanja wa Mkapa walishuhudia ubao ukisoma KMC 0-1 Yanga na mtupiaji alikuwa ni Clement Mzize.

KMC ilipenya kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2 Mbeya City ambayo hii itashiriki Championship.

Mbeya City kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Sokoine ilipata ushindi wa mabao 2-1 na mchezo wa pili wa kumsaka mshindi ikashuhudia ubao wa Uwanja wa Uhuru ukisoma KMC 2-0 Mbeya City.

Hivyo ni rasmi kuwa KMC WanaKinoBoys bado wapo ndani ya ligi na wanatarajia kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi hicho.

Ni nafasi ya 13 iligotea na kukusanya pointi 32 baada ya kucheza mechi 30.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here