Home KIMATAIFA KOCHA YANGA ATAMBULISHWA KWENYE TIMU MPYA

KOCHA YANGA ATAMBULISHWA KWENYE TIMU MPYA

0
Nabi

NI rasmi Nasreddine Nabi (57) aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga ametangazwa kuwa kocha wa mabingwa wa Morocco AS FAR Rabat.

Ni mkataba wa miaka miwili amesaini kwa ajili ya kuwatumikia mabingwa hao wa Morocco.

Nasreddine Nabi ambaye ni raia huyo wa Tunisia alitangazwa kuachana rasmi na Yanga mwishoni mwa msimu wa 2022/23 ambapo alikuwa akihusishwa na klabu mbalimbali hapa barani Afrika ikiwa ni pamoja na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Esperance de Tunis ya nchini kwao Tunisia pamoja na AS FAR Rabat.

Hatimaye AS FAR Rabat imefanikiwa kuinasa saini ya kocha huyo aliyekuwa ndani ya Yanga.

Aidha, Ikumbukwe kwamba alifanikiwa kuifikisha Yanga kwenye fainali za michuano ya shirikisho msimu wa 2022/23 huku ikishuhudiwa USM Alger ya Algeria ikitwaa ubingwa wa michuano hiyo, lakini pia kwa misimu miwili mfululizo ambayo Nabi amekuwa na Yanga,walikuwa imara kwenye mechi za mashindano.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here