Uongozi wa Singida Fountain Gate upo katika hatua nzuri katika mazungumzo ya siri na nyota wa sasa wa Yanga Bernad Morrison
Katika mazungumzo hayo Morrison ameripotiwa kuonesha nia ya kumwaga wino kunako dirisha kubwa la usajili na muda wowote kufuatia kufunguliwa kwa dirisha hilo huenda akatangazwa kama mkulima wa Alizeti
Morrison atasaini mkataba wa mwaka mmoja na chaguo la kuongeza mkataba baada ya kutamatika kwa mkataba wake huku maslahi yake yakitajwa kuongezeka maradufu na yale ya sasa
Ikumbukwe Singida Fountain Gate itashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao,hivyo tutegemee lolote katika hili.
Unaipa Singida FG ama Big NO?
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE