Home KITAIFA MTAMBO WA MABAO HUU HAPA KURITHI MIKOBA YA MAYELE

MTAMBO WA MABAO HUU HAPA KURITHI MIKOBA YA MAYELE

0
Hafiz Konkoni, Young Africans

KUTOKA Ghana Hafiz Konkoni  mwenye umri wa miaka 23 alikuwa anakipiga Club ya Bechem United ya Ghana amesaini dili jipya Yanga.

Hafiz msimu wa 2022/23 rekodi zinaonyesha kuwa kwenye Ligi Kuu nchini Ghana aligotea nafasi ya pili kwa wanaowania Tuzo ya Mfungaji bora kwa kufunga mabao 15 na pasi tatu za mabao.

Nyota huyo alipata nafasi ya kucheza katika michezo 26 kwenye ligi atakuwa kwenye changamoto mpya Yanga.

Ni dili jipya amesaini ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamond akitajwa kueba mikoba ya Fiston Mayele ambaye huenda akaibukia Pyramid FC ya Misri.

Mayele ni mfungaji bora ndani ya Yanga msimu wa 2022/23 alipotupia mabao 17 na ana tuzo ya mchezaji bora wa msimu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here