Home KITAIFA MWAMBA HUYU HAPA ALIYECHUKUA MIKOBA YA MAYELE

MWAMBA HUYU HAPA ALIYECHUKUA MIKOBA YA MAYELE

0

Klabu ya Young Africans imemsajili Mshambuliaji Hafiz Konkoni raia wa Ghana kwa mkataba wa miaka miwili na inaelezwa ndio mbadala wa Fiston Mayele.

Mshambuliaji huyo kutoka timu ya Bechem United inayoshiriki Ligi Kuu ya Ghana yupo vizuri katika kupachika mabao kama ilivyokuwa kwa Fiston Mayele aliyeuzwa kwenye klabu ya Pyramids FC ya Misri.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Young Africans, zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo alitarajiwa kuwasili nchini jana Jumapili (Julai 23) na leo Jumatatu (Julai 24) atatambulishwa rasmi tayari kujiunga na wenzake kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ngao ya Jamii na michuano mingine.

“Tumeshakamilisha kila kitu na mchezaji yupo njiani tunatarajia kumpokea leo (jana) na kesho tutamtambulisha na kuingia kambini rasmi”

Mshambuliaji huyo kabla ya kujiunga na Bechem ya Ghana aliwahi kucheza soka la kulipwa kwenye timu mbili za Alsancak Ye ilova na Baf Ülkü Yurdu za Kaskazini mwa Cyprus pia amewahi kuitwa mara moja timu ya taifa ya Ghana.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here