Home KITAIFA SIMBA YAWEKA WAZI ISHU YA KUACHANA NA BANDA

SIMBA YAWEKA WAZI ISHU YA KUACHANA NA BANDA

0

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Imani Kajula amesema kuwa klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha mazungumzo na makubaliano baina yao na mchezaji wao, Peter Banda raia wa Malawi ili kumruhusu kuondoka klabuni hapo.

Simba wanatakiwa kuondoa mchezaji mmoja wa kimataifa ili kubakisha wachezaji 12 kwa mujibu wa kanuni za TFF kwani mpaka sasa wachezaji wa kimataifa ndani ya kikosi hicho ni 13.

“Tupo kwenye hatua ya mwisho wa mpango wetu juu ya Peter Banda na ukishakamilika tutawajuza wote ila kwasasa tunaelekea katika hatua za mwisho tutawaambia yapi makubaliano yetu kati ya Simba SC na Peter Banda au anaelekea wapi.”

“Ila pia sisi sio kama wenzetu wakiachana na wachezaji wao hawasemi sisi tunasema imekuaje na kwa makubaliano yapi ndio maaana mmeona kwa Pape Osmane Sakho ameondoka tumesema ameondoka na tumemuuza,” amesema Imani Kajula.

Banda anatajwa kuwa huenda akasajiliwa na moja ya vilabu nchini Ufaransa kama ilivyokuwa kwa mwenzake Pape Ousmane Sakho ambaye ameshaondoka klabuni hapo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here