Home KITAIFA SIRI IMEFUJA SABABU ZA SIMBA KUMTEMA KIPA WAO MBAZILI

SIRI IMEFUJA SABABU ZA SIMBA KUMTEMA KIPA WAO MBAZILI

0
simba

SIMBA imefanya maamuzi magumu ya kumpiga chini kipa Mbrazili Jefferson Luis aliyesajiliwa hivi karibuni kwa madai ya kuwa majeruhi.

Japo klabu haijatoa taarifa lakini inaelezwa Jefferson amepata majeraha makubwa, hivyo amesitishiwa mkataba kwani atakuwa nje kwa muda mrefu.

Chanzo chetu cha kuaminika kinasema kwamba Jefferson alisajiliwa huku akiwa na tatizo la misuli nyuma ya paja lililogundulika juzi mazoezini, huku jina lake likiwa tayari katika usajili wa CAF.

“Ni kweli amegundulika na tatizo hilo, anaweza kukaa nje kwa muda mrefu ila siwezi kusema moja kwa moja kama mkataba utavunjwa au lah! Maana maamuzi hayajafikiwa,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here