Home KITAIFA WALIOIVURUGA YANGA BADO WAPO SANA

WALIOIVURUGA YANGA BADO WAPO SANA

0

NYOTA wawili walioivuruga rekodi ya Yanga kufikisha mechi 50 bila kufungwa ndani ya ligi bado wapo ndani ya Ihefu baada ya kuongezewa mkataba.

Yanga ilicheza mechi 49 bila kufungwa kwenye mechi za ligi ilipokutana na Ihefu ilishindwa kupata sare ama ushindi zaidi ya kufungwa mabao 2-1 na kutibua rekodi hiyo iliyoandikwa na Yanga.

Wafungaji kwenye mchezo huo ni Lenny Kissu na Nivere Tigere ambao wote wanauhakika wa kubaki ndani ya ligi msimu ujao.

Peter Andrew Ofisa Habari wa Ihefu amesema: “Mlinzi bora Lenny Kissu naye atakuwepo mbali na huyo pia kiungo Nivere Tigere Mr Freekik ataendelea kubaki Uwanja wa Highland Estate.”

Wengine ambao wataendelea kubaki Ihefu ni nahodha Rafael Daud, Jaffary Kibaya na wengine wapya wanatarajiwa kutambulishwa hivi karibuni.

Mbali na hao watibuaji rekodi ya Yanga pia Rashid Juma, Juma Nyosso nao wataendelea kubaki ndani ya timu hiyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here