Home KITAIFA AZAM FC WATEMBEZA MKWARA HUU, WANA JAMBO LAO

AZAM FC WATEMBEZA MKWARA HUU, WANA JAMBO LAO

0
HASHEEM Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wanaoibeza timu hiyo watakutana na balaa kwenye ligi na mashindano mengine.

HASHEEM Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wanaoibeza timu hiyo watakutana na balaa kwenye ligi na mashindano mengine.

Msimu wa 2022/23 Azam FC iligotea nafasi ya tatu kwenye ligi na lishuhudia Yanga ikitwaa taji la ligi.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo iligotea nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Ngao ya Jamii ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 Singida Fountain Gate watupiaji wakiwa ni Prince Dube na Abdul Suleiman, (Sopu).

Azam FC kwenye Ngao ya Jamii mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkwakwani.

Yanga inayonolewa na Miguel Gamondi ilipata ushindi kwa mabao ya Aziz KI na Clement Mzize.

Ibwe amesema kuwa wapo ambao walikuwa wakisema kuwa timu hiyo haina ubora lakini kupitia mchezo wa pili waliona picha halisi.

“Kupoteza mchezo wa kwanza wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga haina maana kwamba hatuna kikosi imara. Bahati nzuri kulikuwa na mechi ya pili iliyokuja na picha tofauti na waliokuwa wanabeza wameona ubora uliopo.

“Tunahitaji kufanya vizuri kwenye mashindano ambayo tunashiriki hilo lipo wazi tutapambana kufanya hivyo na mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi kwenye kila hatua,” amesema Ibwe.

Mchezo wa kwanza kwenye ligi kwa Azam FC unatarajiwa kuwa dhidi ya Kitayosce leo Agosti 16 wakiwa na jambo lao saa 8:00 mchana

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here