Home KITAIFA AZAM YATUMA SALAMU SIMBA, YANGA

AZAM YATUMA SALAMU SIMBA, YANGA

0
AZAM

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Azam ya Dar es Salaam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ , amesema Azam ipo kwenye mradi wa miaka mitatu kuijenga timu tishio kwa michuano ya ndani na kimataifa.

Zaka ameyasema hayo katika mahojiano maalumu kuelekea mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tabora United utakaopigwa leo katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

“Tunaijenga Azam kuja kutawala ‘dominant’ wa nchi kufikia 2026, ambapo tutakuwa tukichukua makombe mfululizo,” amesema Zaka.

Ofisa huyo pia ameelezea malengo ya klabu yao kuelekea michuano ya kimataifa, ambapo wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).

“Sisi hatujawahi kufika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika, kwa hiyo msimu huu wa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, malengo yetu ni kufika hatua ya makundi,” amesema Zaka.

Kwa muda mrefu sasa soka la Tanzania limekuwa likitawalia na klabu za Simba na Yanga, ambazo pia katika michuano ya kimataifa zimekuwa zikifanya vizuri.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here