Home Uncategorized BAADA YA JANA KUUMIA DK YA 6 TU…..HALI YA SKUDU IKO HIVI…YANGA...

BAADA YA JANA KUUMIA DK YA 6 TU…..HALI YA SKUDU IKO HIVI…YANGA WAVUNJA UKIMYA…

0
yanga

UONGOZI wa Yanga umeshusha presha ya mashabiki wa timu hiyo baada ya hali ya kiungo wao Mahletse Makudubela (Skudu) yupo fiti baada ya juzi kushindwa kuendelea na mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii.

Kuumia kwa nyota huyo kumekuwa na taharuki kubwa kwa mashabiki wa timu hiyo, Skudu ambaye alicheza dakika sita baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Crispin Ngushi, mchezo huo uliochezwa, Mkwakwani.

Daktari wa Yanga, Moses Etutu, alisema nyota huyo anaendelea vizuri baada ya kupata maumivu ya makali ya goti na kukimbizwa katika zahati ya mtu binafsi karibu na uwanja huo.

Alisema walimpeleka hospitali mchezo huyo na kufanyiwa vipimo lakini bahati nzuri alionekana hajavunjika wakaruhusiwa kurudi naye katika hoteli ya Maunt Usambara ambayo wamefikia.

“Tulikuwa na wasiwasi baada ya matibabu hayo Skudu anaendelea vizuri, mwanzo alikuwa na maumivu sana hali iliyosababisha kumpeleka hospitali, lakini ameamka vizuri anaendelea na matibabu.

Kwa sasa atakuwa chini ya uangalizi na kutumia dawa za kupunguza maumivu, ninaimani kwa muda mfupi atakuwa sawa , mashabiki wasiwe na hofu juu ya nyota huyo,” alisema Etutu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here