Home KITAIFA BAADA YA YANGA KUWAFUNGA KWA TABU WADJIBOUTI, DICKSON JOB MAGUMU WALIYOPITIA

BAADA YA YANGA KUWAFUNGA KWA TABU WADJIBOUTI, DICKSON JOB MAGUMU WALIYOPITIA

0
Dickson Job

BEKI wa Yanga, Dickson Job amesema nidhamu kwa wapinzania wao AS Al Sabieh (Asas FC) , kimepelekea kupata ushindi wa mabao 2-0 katkka mchezo huo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Job alisema Asas FC haikuwa timu kibonde kama ilivyodhaniwa na baadhi ya watu kwa sababu ya kuwa inashiriki ligi ya Djibouti.

Alisema mechi hiyo haikuwa rahisi kwa sababu Asas FC ni timu nzuro waliingia kuwaheshimu na kucheza kwa nidhamu kubwa na kufanikiwa kupata matokeo mazuri.

“Hadi kufika hatua hii ujue ni mabingwa wa Djibouti, hatukuwabeza tulicheza kwa nidhamu kubwa, tuliwaheshimu ndio sababu ya kupata matokeo haya,” alisema Job.

Alisema anaimani ulikuwa mchezo mzuri na ushindani mkubwa kwa sababu wapinzani wao walionyesha ushundani mkubwa licha ya kupata ushundi wa mabao 2-0.

Adiha katika hatua nyingine, KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamondi amesema hakufurahishwa na jinsi wachezaji wake walivyocheza na kuahidi kufanyia marekebisho kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi As Al Sabieh ya Djibouti.

Katika mchezo wa kwanza ambao Yanga walikuwa ugenini katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi na maruadiano Yanga watakuaa nyumbani katika dimba hilo mchezo utakaopigwa Agosti 27 mwaka huu

Gamondi alisema hajafurahishwa na jinsi timu ilivyocheza kipindi cha kwanza kwa kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.

Alisema anatarajia kufanya marekebisho makubwa kuelekea mchezo wa marudiano na kuwa bora zaidi na kucheza vizuri zaidi baada ya kuona ubora na madhaifu ya wapinzania wao.

“Tumecheza vizuri kipindi cha pili, ninaimani mechi ijayo itakuwa nzuri kwa sababu sasa nimewaona wapinzani wetu na tunatarajia kupata matokeo mazuri zaidi mchezo wa marudiano,” alisema kocha huyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here