Home KITAIFA DILI LA CAICEDO LINAKWENDA KUANDIKA REKODI MATATA

DILI LA CAICEDO LINAKWENDA KUANDIKA REKODI MATATA

0
Moises Caicedo

IKIWA dili lake litakamilika rekodi mpya inakwenda kuandikwa Uingereza kwa gharama ambazo zitatumika kuipata saini ya Moises Caicedo kutoka Brighton kwenda Chelsea.

Imeelezwa kuwa kuna nyongeza katika mkataba imeongezwa na kufikia dili lenye thamani ya pauni milioni 115 na

Chelsea wamekubali ada ya rekodi ya Uingereza ya pauni milioni 115 na Brighton kwa ajili ya Caicedo.

Kutokana na kufkia makubaliano hayo nyota huyo atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kukamilisha uhamisho wake.

Ikumbukwe kwamba alikataa nafasi ya kujiunga na Liverpool iliyokuwa inapewa nafasi ya kuipata saini yake yeye alibainisha kwambwa anapendelea kuhamia Stamford Bridge.

The Blues wanadaiwa kulipa pauni milioni 100 za awali, pamoja na pauni milioni 15 katika nyongeza zinazohusiana na utendaji.

Ada hiyo inazidi pauni milioni 107 ambazo Chelsea ililipa kwa Enzo Fernandez wakati wa kuvunja rekodi ya uhamisho wa Uingereza mwezi Januari.

Kulingana na David Ornstein, nyongeza katika mkataba waliokubaliwa na Chelsea zinaonekana kuwa ‘zinazoweza kufikiwa’ sana.

Brighton wanawatarajia haraka kwani Chelsea walitoa pesa za uhakika zaidi kuliko Liverpool.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here