Home KITAIFA GAMONDI ATOA TAARIFA MUHIMU KWA WANAYANGA WOTE “RAHA KWENDA MBELE”

GAMONDI ATOA TAARIFA MUHIMU KWA WANAYANGA WOTE “RAHA KWENDA MBELE”

0
Gamondi

Kocha wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao dhidi ya Maafande wa JKT Tanzania utakaopigwa kesho Agosti 29, 2023 katika dimba la Azam Complex Chamazi.

Kocha huyo anasema falsafa yake ni kusakata soka safi bila kujali anacheza na timu gani lakini anaheshimu kila mpinzani anaekutana naye.

“Licha ya kwamba tunajua mpinzani wetu ni timu iliyopanda daraja, wana wachezaji wenye uzoefu hivyo hatupaswi kuichukulia kama timu dhaifu, ninafikiri kesho tunapaswa kujiamini na kufunga magoli mengi” amesema Gamondi.

Mchezo huo utakuwa ni wa pili kwa Yanga kwenye ligi kuu ambapo mchezo wa kwanza waliibugiza Kmc mabao 5-0.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here