Home KITAIFA ISHU YA SINGIDA KUSHIRIKIANA NA YANGA KUIMALIZA SIMBA IKO HIVI

ISHU YA SINGIDA KUSHIRIKIANA NA YANGA KUIMALIZA SIMBA IKO HIVI

0
simba

Klabu ya Singida Fountain Gate imetolea ufafanuzi taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa inshirikiana na Klabu ya Yanga kuelekea fainali ya Ngao ya Jamii leo kati ya Yanga na Simba Sc kwenye Dimba la CCM Mkwakwani Tanga.

Taarifa hiyo inakuja baada ya kusambaa kwa picha zikiwaonyesha baadhi wachezaji wa Yanga na wale wa Singida FG, kocha wa Singida Hans Van Pluijm na Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi wakiwa pamoja katika uwanja wa mazoezi wa TFF Tanga, jana Jumamosi.

Taarifa iliyotolewa na Singida FG imeeleza;

Tumesikitishwa na taarifa ya upotoshaji wa makusudi inayosambaa kwa kasi kuwa Singida Fountain Gate FC inashirikiana na Yanga SC dhidi ya Simba SC katika fainali ya leo ya Ngao ya Jamii.

Singida FG haihusiki na chochote katika mechi ya fainali leo isipokuwa kuelekeza nguvu zetu kwenye mechi yetu dhidi ya Azam FC kuwania nafasi ya tatu.

Ukweli ni kwamba Yanga na Singida FG zilikutana wakati timu yetu ikitoka baada ya kumaliza mazoezi kwenye uwanja wa mazoezi wa TEF jijini Tanga ambako klabu zote shiriki zinafanyia mazoezi.

Picha zinazosambaa za Kocha wetu na Kocha wa Yanga pamoja na wachezaji zinatumiwa tu na watu wenye nia ovu ya kuleta mfarakano kati yetu na Simba SC.

Tunawasihi mashabiki na wadau wetu kupuuzia uzushi huo na kuelekeza nguvu kwenye mechi yetu dhidi ya Azam FC. Asante sana.

Olebile Sikwane, Mtendaji Mkuu Singida Fountain Gate FC.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here